HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=138601",
"previous": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=138599",
"results": [
{
"id": 1402411,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402411/?format=api",
"text_counter": 168,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui South, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
"speaker": {
"id": 13374,
"legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
"slug": "richard-ken-chonga-kiti"
},
"content": " Thank you very much, Hon. Deputy Speaker. I will just make a few comments on this Bill. Before I do, I would like to encourage more support to Chairpersons of Committees so that they do not struggle when moving their Bills for Second Reading. I state that as a third-term Member. It is extremely important to support them. This is a very important Bill moved by Hon. Kitany. I listened to her as she moved and the Seconder. The purpose is to ensure that counties do not have different systems of licensing so that we provide as much support as possible to investors. Investors get attracted to a country called ‘Kenya’. As they do their feasibility studies, they realise that Kenya also has counties. At times, they find themselves operating in more than one county. This Bill encourages counties to have a very simple system of licensing, possibly a uniform one, so that they do not struggle. It is very important that it is passed. Investors will invest in different counties without struggling to ensure they follow different systems from one county to the other. I would like to focus on payments, especially levies on roads. When investors are transporting goods, for example, from Nairobi to Kitui, they find themselves paying levies to Nairobi City County. On the way, if they use Mombasa Road they will pay to Makueni County, and then as they cross to my constituency pay levies to Kitui County. Those are three levies. This is a matter that needs to be looked at because it increases the costs of doing business. All these costs are levied on customers. If we have an easier way of making it easier to do business, we will have more investors and ensure our counties grow. Counties will collect more funds and have more development. It is through these companies constructing in our villages that we can get more and more young people employed. This is a Bill that must be supported. Thank you very much for the opportunity. I support."
},
{
"id": 1402412,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402412/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Deputy Speaker",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Member for Likoni, Hon. Mishi Mboko."
},
{
"id": 1402413,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402413/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono Mswada huu ambao unazungumzia leseni na kuhakikisha taratibu zake ziko na usawa katika Jamhuri yetu ya Kenya. Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu litawalinda watumiaji wa bidhaa na huduma, kwa wale ambao hawajaelewa, the consumers, ili waelewe taratibu zinazofuatwa kupata leseni. Kuna taratibu tofauti katika kila kaunti. Tukiwa na taratibu tofauti, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
},
{
"id": 1402414,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402414/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "mara nyingi tunawaumiza watumiaji na waekezaji ambao wanakuja kwenye kaunti zetu kuboresha uchumi. Mswada huu umezungumzia wakati kaunti inataka kubadilisha malipo ya leseni lazima ifanye mkutano na washikadau, ile tunaita kwa Kiingereza public participation. Wazungumzie swala lile kwamba wamebadilisha yale malipo. Hivi sasa unapata katika kaunti nyingi, wanaamka tu na wanasema pengine kwamba kuegeza gari limepandishwa, na mtalipa pesa hizi. Ama ile pesa ya cess imepandishwa, na mtalipa pesa hizi, pasi na kuwahusisha wale washikadau. Vilevile, Mswada huu umezungumzia kwamba yale malipo yatakayowekwa hayatakuwa ya kuumiza yule mtumiaji ama muwekezaji. Yatamwezesha yule mwekezaji ama mtumiaji wa bidhaa. Iwapo mtu anataka kupata zaidi ya leseni moja, Mswada huu unaonyesha taratibu ambazo zitafuatwa ndio asiwe na ugumu wa kuweka yale maombi ya leseni. Kwa hivyo, kutakuwa na taratibu za usawa, pasi na kuumiza watumiaji. Pia, Mswada unasema huduma na bidhaa zinapaswa ziwe bora. Sio eti kutakuwa na huduma tu ambayo si bora, ama kutakuwa na bidhaa ambazo si bora. Lazima ziwe ni bidhaa na huduma bora. Vilevile kutakuwa na kanuni ama alama ya siri, ile kwa Kiingereza tunaita code . Kutakuwa na alama za siri tofauti katika kila leseni ambayo mtu atakua ameomba. Tukiwa na moja tu, hapo huwa tunakuwa na mchanganyiko na tunaleta shida kwa wale watumiaji ama waekezaji. Tutakuwa na hizo alama za siri ama kanuni tofauti katika kila kaunti. Haiwezi kuwa kaunti ya Kilifi na Nakuru itakuwa na hiyo alama moja. Tukifanya hivyo, tunaleta tofauti ama sintofahamu kwa wale watumiaji wakati wameweka maombi ya kupata leseni zile. Mswada huu umerahisisha ama kuweka mambo wazi na umeleta uwajibikaji katika kupata leseni. Utumiaji unaeleza malipo ya leseni yatakavyolipwa yatakuwa ni kwa njia gani. Tumekuwa na shida sana. Wananchi wengi wanalia. Unapata tu mambo yanaongezwa kila uchao. Tukiangalia hali yetu ya kiuchumi vile ilivyo, japokuwa sasa hivi tunaona mambo pengine huenda yakabadilika yakawa mazuri, Wakenya wengi bado wanapata shida sana kwa sababu hakuna sheria mwafaka kama hizi. Tukiwa na sheria ya kitaifa ambayo itakuwa imesimamia kaunti zote, basi hakuna gavana ama kaunti ambayo itaenda kinyume kwa sababu sheria ni msumeno na inakata mbele na nyuma. Lazima ifuatwe. Mbali na yale mambo mengi ambayo yatafanya, pia katika mambo yetu ya mazingira, ile tunaita kwa Kiingereza environmental protection, sheria hii itachunga mazingira. Mswada huu pia umezungumzia zile taratibu ama njia zitawekwa ziwe ni nyepesi na wananchi apate maelezo. Tunasema access to information ; awe anaweza kupata maelezo pasi na kuwa na vizuizi. Katika jambo hili, kuna mambo mengi sana ya ufisadi. Unapata mtu anaambiwa akitaka leseni ama fomu lazima kwanza achotee mtu. Tunataka Mswada huu uwe na wepesi wa kupata maelezo na taratibu zinazohusika katika mambo ya kupata leseni. Nimefurahishwa sana na jambo hili kwa sababu litahusisha washikadau. Kwa hivyo, hakutakuwa na pahali mshikadau atalalamika na aseme hakujua au hakuhusishwa mambo yanapoenda kwa njia ambayo haikuwa imepangwa. Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa sababu unaenda kwa mkutano mwingine muhimu. Niwaambie Wabunge wenzangu, kesho Rais atakuwa katika maeneo ya Bunge Tower kutufungulia jumba lile kirasmi. Nyote mnaalikwa. Poleni, haikuwa mada hiyo, lakini ninawaalika. Ahsante."
},
{
"id": 1402415,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402415/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Deputy Speaker",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Member for Wundanyi, Hon. Danson Mwashako. Member for Matuga, Hon. Kassim Tandaza."
},
{
"id": 1402416,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402416/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "scene",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Technical hitch)"
},
{
"id": 1402417,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402417/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia fursa hii niweze kuchangia mjadala huu muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya hasa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
},
{
"id": 1402418,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402418/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "baada ya kupitishwa kwa Katiba 2010. Licha ya kuwa Katiba ilileta mambo mengi mazuri, pia ilileta changamoto. Ilisisitiza sana kwamba kaunti zetu zitengeneze fedha za ndani kwa ndani licha ya ule mgao ambao unatoka kwa Serikali kuu. Hii ilifanya kaunti nyingi kufikiria njia za kuokota pesa kutoka kwa wananchi. Moja ya njia hizo ni kutoa leseni kwa utafutaji wa rasilimali ambazo zinatoka sehemu mbalimbali."
},
{
"id": 1402419,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402419/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Kama ilivyopendekezwa katika huu Mswada ambao ninaunga mkono, ni jambo la kuhuzunisha kwamba biashara inakuwa ngumu kufanya. Wakati mwingine hata sio biashara tu, hata usafiri. Lori ambalo hata halijabeba kitu likipita kaunti moja hadi nyingine imekuwa ni kama kupitia nchi moja mpaka nyingine. Kwamba, lazima liwe na vibali vya kaunti ambako linaenda licha ya kutozwa ushuru wa ule mzigo ambao limebeba. Hivi vibali ambavyo kaunti zinatoa kwa magari ya mizigo si halali. Tunajua kuwa katika nchi hii, tunayo Wizara inayohusika na kutoa vibali nayo ni Wizara ya Uchukuzi. Na kama ni insurance basi inakua ni ya Kenya nzima. Lakini kaunti zingine zimeweza kutoa vibali vya kadi na kubandika katika magari, kuonyesha gari hili linaruhusiwa kufanya biashara katika eneo lao. Jambo hili halina msingi, bali ni hali ya kuhangaisha wanabiashara. Ni hali ya kufanya bidhaa ziwe ghali zaidi ilhali tunazungumzia ni vipi wananchi wa kawaida wanaweza kupata afueni kibiashara. Nchi hii ni moja na kaunti zililetwa kwa sababu ya kupeleka huduma mashinani. Lakini saa hizi zimekuwa zikiwafinya watu kupitia hizi sheria zao. Kutoka maeneo ya Kwale kuingia Mombasa ni kama ambaye unavuka mpaka wa Lunga Lunga kutoka Kenya kwenda Tanzania. Kwa hivyo, Mswada huu ni muhimu na unahitaji kuungwa mkono na kupitishwa haraka inavyowezekana ili biashara zifanywe bila matata ama pingamizi yoyote."
},
{
"id": 1402420,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402420/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Naibu Spika, jambo jingine ambalo ni la kuhuzunisha ni ufadhili. Kwa mfano, pale Kaunti ya Kwale labda ufadhili utapitia Bandari ya Mombasa ambayo ni kaunti nyingine. Kwa mfano, mtu amenuia kusaidia shule za Kwale kwa kuzipa kompyuta ama vitu ambavyo vitatumika katika darasa. Kisha gari linapofika mpakani kati ya Kaunti ya Mombasa na Kwale pale Likoni yule mfadhili analazimika kulipa ushuru tena licha ya kuwa pengine ashalipa kwa Serikali kuu bandarini. Kaunti bado inahitaji ushuru tena ulipwe ili vyombo viweze kuingia ilhali bidhaa si za biashara - ni mtu binafsi amejitolea kutoa ufadhili kusaidia watu wetu. Lakini yule afisa ambaye amewekwa pale kwenye kituo cha cess anashauri kwamba ni lazima gari lolote linalopita hata ingawa ni la ufadhili lilipe ushuru la sivyo atalifungia. Inabidi mwenye gari azungumze na mstahiki gavana ama mkubwa ambaye anahusika, ili gari liachiliwe. Sisi kama Bunge tuna jukumu la kuona kwamba hali tata kama hizi haziwezi kuendelea. Ikiwa watatoza ushuru basi mtu akiwa ametoka Kilifi akienda Kwale, akilipa ushuru Kaunti ya Kilifi, aweze kubeba risiti kuonyesha tayari ashalipia katika gatuzi moja na anastahili kuubeba mzigo mahali popote pale Kenya. Hii ni kwa sababu nchi ni moja. Alikotoa bidhaa yule mfanya biashara amelipishwa, pengine, Ksh200 na akifika Mombasa analipishwa Ksh800. Akivuka Kwale analipishwa labda Ksh1,000. Je, atapataje faida yake?"
}
]
}