HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=138804",
"previous": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=138802",
"results": [
{
"id": 1404441,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404441/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu wa Tume ya Ardhi tukizingatia ya kwamba Wakenya walipiga kura ya kubadilisha Katiba. Mojawapo ya mabadiliko ilikuwa kuunda Tume ya Ardhi. Sababu ya kuunda Tume ya Ardhi ni kuwa kulikuwa na malalamiko mengi sana kuhusu dhuluma za kihistoria za ardhi. Kifungu 62 cha Katiba kinasema kuwa ardhi ya umma itakuwa chini ya usimamizi wa Rais kupitia Tume ya Ardhi. Hivyo basi, Tume hii ni muhimu sana. Kifungu 67 kimezungumzia kuanzishwa kwa Tume ya Ardhi na majukumu yake, ikiwemo usimamizi wa ardhi za umma. Kati ya majukumu hayo, kuna kusimamia ruzuku. Kwa wale ambao hawataelewa, ruzuku ni grants . Kwa hivyo kuna suala la kuzisimamia na kutathmini kama ugavi wake ulikuwa sawa ama ulikuwa na shida. Muda ambao ulipatiwa Tume ya Ardhi kuangalia masuala haya ulikuwa miaka mitano. Sasa hivi, tunachelea ya kwamba Tume itakosa mamlaka hayo. Lakini bado tuko na matatizo nyeti sana haswa mambo ya dhuluma inayotokana na ardhi. Machafuko mengi sana katika taifa letu la Kenya yalikuwa kwa sababu ya shida zilizotokana na umilikaji wa ardhi. Hii ndiyo sababu tulisema tuwe na Tume itakayosaidiana na Wizara ya Ardhi katika kutathmini suala hili la matatizo ya ardhi na kuangalia ruzuku. Katika sehemu nyingi za taifa la Kenya, kuna watu ambao walipatiwa ruzuku kwa njia za kisiasa na ambazo hazikuwa mwafaka wala sawa. Katika ardhi zile, watu hawapatikani, hawaonekani na hawajulikani wako wapi. Wakati Serikali inajaribu kutatua matatizo ya maskwota kwa kutumia ardhi kama hizi, inakuwa ni shida kwa sababu wale waliopatiwa hawapatikani. Lazima Tume ya Ardhi iendelee na kazi yake ili tuweze kuangalia ruzuku hizi zilipeanwa kwa njia gani. Je, wale waliopatiwa ruzuku hizi bado wako ama hawako? Na kweli The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
},
{
"id": 1404442,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404442/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "walikuwa ni walengwa ama ni wale wale ambao walipata kupitia njia za kisiasa zisizo sawa? Hii itatusaidia kutathmini hali. Vile vile, Mhe. Owen amekizungumzia Kifungu 15(3) na kusema lazima kifutwe. Hii ni kwa sababu kikiwa hapo, kitakuwa pingamizi katika kutekeleza shabaha za Tume ya Ardhi. Wakenya walizungumzia kuwepo kwa Tume ya Ardhi kwa sababu Wizara ilikuwa hapo kwa miaka mingi sana na haikuweza kutathmini, haswa kuangalia zile dhuluma za kihistoria za mambo ya ardhi. Kwa mfano, Serikali iliangalia ile ardhi ya Mazrui iliyoko sehemu za Kilifi na ikasema kuwa itapeana pesa kwa wahusika ili kusaidia maskwota walio pale wapewe ardhi. Iwapo Tume ya Ardhi itasitishwa kufanya kazi yake, mambo kama haya ambayo yamefanyika yatakuwa ni shida. Itabidi tena turudi mwanzo ili tuone jinsi ya kutatua tatizo hili nyeti. Ukiangalia sehemu ya Bonde la Ufa, kuna matatizo mengi ya ardhi kupitia dhuluma za kihistoria. Pia Pwani, matatizo kama hayo ni mengi. Katika sehemu za kati nchini, vile vile tumeona matatizo hayo. Kwa jumla, Kenya nzima inayo haya matatizo."
},
{
"id": 1404443,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404443/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "scene",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "[The Speaker (Hon. Moses Wetang’ula) left the Chair]"
},
{
"id": 1404444,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404444/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "scene",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "[The Deputy Speaker (Hon. Gladys Boss) took the Chair]"
},
{
"id": 1404445,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404445/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Nilikuwa katika Kamati ya Ardhi katika Bunge lililopita. Najua, hadi sasa, kesi ambazo bado hazijaamuliwa ili kuwasaidia Wakenya ni nyingi mno. Hata tukitathmini hali hivi sasa tuchunguze Tume imetufanyia kazi ngapi katika kutatua dhuluma za kihistoria za ardhi na kutatua mambo ya ruzuku, tutapata kwamba bado shida ni nyingi na bado hatujapata uamuzi wowote. Tusianze kuvunja nguvu ama zile Tume ambazo sisi wenyewe tuliunda kupitia Katiba ya mwananchi. Tulisema kwamba Wanjiku aliongea, Kadzo ameongea, na Achieng’ ameongea. Kwa hivyo, waliongea kwa sababu za kimsingi, haswa kuhusu suala la ardhi. Mhe. Naibu Spika, suala la ardhi limeleta maafa katika taifa letu la Kenya. Limeleta sintofahamu katika jamii, haswa ardhi za umma. Hizo siku za nyuma, watu hawakuwa na uwezo wa kutengeneza stakabadhi ama kuziweka katika njia ya kisheria. Watu walikuwa wanajua ardhi ya jamii fulani, ni ardhi yao. Hivyo basi, wale wezi wa mashamba waliweza kufanya mambo ambayo si halali na kupata umiliki wa mashamba ya umma ambayo si mashamba yao. Ni lazima tupatie Tume ya Ardhi nafasi mwafaka na ya kutosha ili Wakenya na jamii zote katika ardhi zetu za umma wapate haki. Iwapo hawatapata haki itakuwa kwamba fedha iliyotumika kubadilisha Katiba ama kuunda Tume imetumika kufanya kazi bure. Zile fedha za ushuru za mwananchi wa Kenya zitakuwa zimeenda pasi na kuwa na faida. Hili ni suala nyeti na lazima tulipatie kipaumbele kwa sababu Katiba yenyewe ishalizungumzia. Kama viongozi wa Bunge, hakuna ambaye hajaletewa matatizo ya ardhi ya dhuluma za kihistoria katika eneo Bunge lake. Tuna matatizo haya kila mahali. Kuna yale maeneo tunajua yalikuwa na matatizo sana, kwa mfano, Bonde la Ufa na ukanda wa Pwani. Jumla, Kenya nzima imekuwa na shida kuhusu ardhi.Tukisema kwamba hili suala tunaliacha, itabidi tuanze tena kutafuta sheria nyingine, kwa mfano, kurudisha jambo hili katika Wizara ya Ardhi ama tutengeneze taratibu nyingine za kusimamia suala hili. Kwa nini turudi nyuma wakati tulikuwa tushaenda hatua fulani ya kuweza kutathmini swala kama hili la dhulma ya kihistoria na kuweza kuzungumzia mambo ya ruzuku?"
},
{
"id": 1404446,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404446/?format=api",
"text_counter": 230,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Vile vile, tunajua kufikia sasa, kuna mambo ya kulipa fidia ambayo yanasimamiwa na Tume ya Ardhi na bado tuna matatizo nyeti. Tuna kesi ambazo hazijapata uamuzi, zimesimama na Wakenya wanatuangalia sana kuona ya kwamba Serikali ilioko mamlakani itaweza kuwapatia afueni Wakenya katika swala hili nyeti la ardhi."
},
{
"id": 1404447,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404447/?format=api",
"text_counter": 231,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Naibu wa Spika, ninamuunga mkono Mhe. Owen Baya kwa kufikiria swala kama hili. Maanake nikiangalia Kilifi kwake, kuna kule sehemu ya Vipingo ambayo kuna ardhi zilitolewa kiholeha ambazo nyingine zilikuwa ni ardhi za umma na hadi sasa watu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
},
{
"id": 1404448,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404448/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "hawajarejeshewa. Tuna wale ambao wanasema ardhi ni zetu lakini hawaonekani. Kwa Kiingereza tunasema absentee landlords. Yote hayo ni katika zile dhulma za ardhi za kihistoria ambazo bado hazijatathminiwa na hatujapata suluhu katika matatizo haya."
},
{
"id": 1404449,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404449/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, ni mwafaka kuweza kuwa na Mswada kama huu, tuupitishe sote kwa jumla pale tulipo kama viongozi wa Bunge hili la Kitaifa. Wakenya wanatuangalia na wamehangaika sana. Ardhi za umma za karibu jamii zote za taifa la Kenya wamepata shida. Asante sana Mhe. Naibu Spika na Mhe. Owen."
},
{
"id": 1404450,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404450/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Deputy Speaker",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Member for Kisauni, Hon. Bedzimba Rashid."
}
]
}