HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=150335",
"previous": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=150333",
"results": [
{
"id": 1521532,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521532/?format=api",
"text_counter": 92,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia kauli mbili ambazo zimeletwa na Sen. Olekina pamoja na Sen. Kibwana. Nitaanza na kauli ya Sen. Olekina. Matatizo yaliyotokea kutokana na uagizaji kutoka nje wa ngano imetokona na kutojua kwa watu wetu kwenye Wizara ya Ukulima na kwenye Wizara ya mambo ya nje. Yale makubaliano yanayofanyika katika vikao vinavyofanyika mara kwa mara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Yale yanayozungumzwa katika vikao vile hayafiki mashinani kwa wananchi. Kamati ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa inafaa iingilie kati kutatua suala hili. Wakulima wa nchi jirani wanajua masoko yao yako vipi. Wakulima wetu hawana habari hizo. Kwa mfano, mara nyingi sukari ya Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA) inaletwa nchini ilhali tuna sukari yetu nchini. Pia mahindi inatolewa sehemu za Malawi kuingia Kenya lakini bidhaa hii inapandwa kwa wingi na hatuwezi kununua kwa bei ambayo Serikali inaamua. Hivi sasa kumechaguliwa wenyeviti wapya wa kamati, inafaa waangalie kwa makini masuala haya ili wananchi wajue taarifa kuhusu mazao. Chakula tunacholima lazima kwanza kinunuliwe hapa kwetu, kile ambacho ni kizuri labda tuuze nje. Tusiwe tunaleta kila zao kutoka nchi, kwani tutawahujumu wakulima wetu. Afya ya akili ni suala ambalo liko wazi katika jamii zetu. Mara nyingi utapata mtu amejiua ama ameadhiri familia yake. Juzi kuna mama mmoja aliua watoto wake watatu hapa Nairobi. Kuna visa vingi kama hizi ambazo zinaripotiwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1521533,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521533/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Mtu kutaka kujitoa uhai haipaswi kuwa hatia. Huyu ni mtu ambaye anaugua afya ya akili na inafaa apewe matibabu na usaidizi ili aepukane na janga hili. Ipo haja ya kufanya marekebisho kwa sheria---"
},
{
"id": 1521534,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521534/?format=api",
"text_counter": 94,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kingi",
"speaker_title": "The Speaker",
"speaker": null,
"content": " Your time is up. Sen. (Dr.) Murango, proceed."
},
{
"id": 1521535,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521535/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ni jambo la fedheha wakati wakulima wanapanda, kupalilia mimea na wanapovuna hawapati walichokuwa wanatarajia. Hili ni jambo linalotokana na makadirio ya bajeti ambayo yanafanywa na Bunge la Kitaifa. Sasa hivi ukiangalia fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kununua mahindi utapata kiasi. Ukiangalia fedha kwenye bajeti ambazo zimetengwa kwa sababu ya ngano, utapata hakuna. Pia hakuna pesa zilizotengwa kusaidia wakulima wa mimea mingine. Wakati wakulima watavuna, hata Mhe. Rais wa nchi atasema nendeni mnunue ngano. Hata hivyo, kwa sababu wakulima hawa hawana soko, utapata kuwa hakuna bajeti. Jambo la kusikitisha ni kuwa hakuna mahali Seneti inahusishwa kikamilifu katika makadirio ya bajeti. Tunafaa kuweka fikira zetu pale ili tuwasidie watu wetu. Bw. Spika, siyo ngano na mahindi pekee. Vile vile kuna sheria zingine katika nchi hii ambazo zinahitaji Waziri kuhakikisha kuwa wakulima wamefaidika. Nchi zingine zinaruzuku wakulima wao kuuza bidhaa zao kwa bei rahisi katika nchi ya Kenya. Sisi tumekuwa kama jaa la kununua kila kitu kwa sababu bei ni rahisi. Ningependa kuzungumzia mazao ya makadamia. Ningependa kwanza kumpongeza Sen. Wakoli ambaye sasa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Tulienda naye kwenye ofisi ya aliyekuwa Waziri, Mhe. Mithika Linturi, kwa sababu kuna sheria ambayo ilikuwa imebuniwa mwaka 2023 ambayo ilikuwa inasema lazima utoe maganda kwenye makadamia kabla ya kuuza katika nchi za nje. Mabwenyenye waliungana na kujenga viwanda vikubwa vikubwa. Maskini lazima angepeleka mazao yake kule. Sasa hivi, kuna sheria hiyo kwamba mkulima hawezi kuuza makadamia nje ya nchi kama haijatolewa maganda. Kwa nini mkulima asiruhusiwe kufuga mbuzi wake mahali kuna nyasi? Kwa nini nilime kisha nikuletee kwa lazima kuambatana na sheria? Hilo ni jambo la kufedhehesha. Ni vizuri wakulima wa ngano waangaliwe haraka iwezekanavyo. Inafaa kuwa hivyo hivyo kwa wakulima wa mahindi na wengineo."
},
{
"id": 1521536,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521536/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kingi",
"speaker_title": "The Speaker",
"speaker": null,
"content": " Senate Minority Leader, proceed."
},
{
"id": 1521537,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521537/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Bw. Spika, ningependa kuunga mkono taarifa hii kuhusu mambo ya ngano. Wakulima wa ngano lazima waangaliwe pia ili mazao yao yanunuliwe katika masoko ya nje. Ni jambo la kusikitisha na madharau kwa wakulima wa ngano kutoonyeshwa kuwa ngano pia ni muhimu. Wakulima wengi hawajui watafanya nini na ngano waliovuna, mmojawao akiwa Sen. Wakili Sigei. Tulipokuwa tukizungumza naye, aliniambia kuwa amevuna ngano nyingi lakini hana mahali pa kuipeleka. Ni kama atapeana bure ama akae nayo na hatimaye iharibike. Taarifa hii ambayo imeletwa na Seneta wa Narok ni muhimu. Wakulima hao wanafaa kuangaziwa ili kuendeleza shughuli zao. Haina haja kuagiza ngano kutoka nje, hali ambayo itakandamiza wakulima wetu. Ni lazima wakulima hao waangaliwe na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
},
{
"id": 1521538,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521538/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "kutetewa na Wizara. Suala hili linafaa kuangaliwa na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo inafaa kuchunguza vizuri na kutupatia mwelekeo."
},
{
"id": 1521539,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521539/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kingi",
"speaker_title": "The Speaker",
"speaker": null,
"content": " Let us go to the next Order."
},
{
"id": 1521540,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521540/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "heading",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "MOTION"
},
{
"id": 1521541,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521541/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "heading",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "CELEBRATING THE LIFE OF THE LATE LEONARD MAMBO MBOTELA"
}
]
}