GET /api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154359
HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "count": 1608389,
    "next": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154360",
    "previous": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154358",
    "results": [
        {
            "id": 1561782,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561782/?format=api",
            "text_counter": 570,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "bodabodas"
        },
        {
            "id": 1561783,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561783/?format=api",
            "text_counter": 571,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Vihiga County, ANC",
            "speaker_title": "Hon. Adagala Beatrice",
            "speaker": null,
            "content": "should be banned, their services are good. Bodaboda riders are doing a good job. They saved Hon. Khalwale that day from being arrested. Therefore, let us not demonise that industry, but hold it with the respect it deserves. It is a good industry that employs our children, except for a few issues that need to be corrected. We leave this to the Cabinet Secretary for Roads, Transport and Public Works to introduce measures and rules, and bring a Bill here The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
        },
        {
            "id": 1561784,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561784/?format=api",
            "text_counter": 572,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Vihiga County, ANC",
            "speaker_title": "Hon. Adagala Beatrice",
            "speaker": null,
            "content": "which can curb lawlessness. There are a few elements that security apparatus should look into. Thugs masquerade as bodaboda riders to rob people or do unnecessary things which spoil that industry. I, however, love the industry. I am very happy in my County because it is coming up. The bodaboda riders have bought land where they want to put up apartments to assist the State Department for Housing and Urban Development meet the requirements of the housing sector. From being bodaboda riders, they are becoming bus and matatu owners. Therefore, let us not demonise the industry wholesomely. It is an industry that needs to be nurtured and protected so that our people can put something on the table in their homes."
        },
        {
            "id": 1561785,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561785/?format=api",
            "text_counter": 573,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Vihiga County, ANC",
            "speaker_title": "Hon. Adagala Beatrice",
            "speaker": null,
            "content": "Thank you, Hon. Temporary Speaker."
        },
        {
            "id": 1561786,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561786/?format=api",
            "text_counter": 574,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Peter Kaluma",
            "speaker_title": "The Temporary Speaker",
            "speaker": {
                "id": 1565,
                "legal_name": "George Peter Opondo Kaluma",
                "slug": "george-peter-opondo-kaluma"
            },
            "content": " Next is the Member for Ganze, Hon. Charo Kazungu."
        },
        {
            "id": 1561787,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561787/?format=api",
            "text_counter": 575,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Ganze, PAA",
            "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
            "speaker": null,
            "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipea nafasi hii ili nichangie huu Mswada. Kwanza, namshukuru na kumpongeza Mhe. Khalwale kwa kubuni Mswada kama huu. Ijapokuwa wamesema hatuwezi kuuondoa, ni Mswada muhimu sana, tukizingatia kwamba sekta ya bodaboda nchini Kenya imechangia pakubwa kuimarisha uchumi wetu."
        },
        {
            "id": 1561788,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561788/?format=api",
            "text_counter": 576,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Ganze, PAA",
            "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
            "speaker": null,
            "content": "Mara nyingi huwa najiuliza, kama sekta ya bodaboda haingekuwa, vijana wetu wengi wanaotoka shule saa hizi, wangekuwa wanafanya kazi gani? Ninavyojua, hali ya uchumi katika nchi yetu si nzuri vile. Vijana wengi wamepata makao katika sekta hii ya bodaboda. Wanajipatia riziki ya kila siku ili kuweza kujiendeleza katika maisha yao. Kwa hivyo, sekta hii imechangia pakubwa katika kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Ganze ni sehemu ya mashambani, yaani rural area . Hakuna barabara. Nafikiri katika Eneobunge lote la Ganze, kilomita za barabara zilizowekwa lami hazifiki hata thelathini. Sisi kama wakaazi wa Ganze tunategemea sana usafiri wa bodaboda kufanya biashara zetu na pia kutoka mahali moja hadi nyingine. Ingekuwa hamna pikipiki, watu wangekuwa wanasafiri kwa miguu au kupitia baiskeli. Mara nyingi, inakuwa vigumu sana kusafirisha bidhaa ama watu, sana sana wagonjwa. Lakini sasa hivi, ukipatikana na shida katika nyumba yako hata kama ni usiku wa manane, ni rahisi kumuita mtu wa bodaboda aje akupeleke hospitalini. Hospitali kule Ganze pia ziko mbali sana. Kila hospitali ni zaidi ya kilomita kumi kutoka kule wananchi wanakoishi na kwa hivyo, kuwafikia kwa urahisi huwa shida. Lakini kwa sababu ya uwepo wa bodaboda, sisi kama wakaazi wa Ganze, tumeweza kupata huduma tofauti kwa urahisi. Sekta hii iko na manufaa mengi sana. Tukianza kuyataja moja baada ya nyingine, pengine tutakesha hapa tukizungumzia mambo haya. Lakini kila kizuri pia hakikosi ubaya wake. Kuna watu wachache ambao wanaharibu jina nzuri la uhudumu wa bodaboda. Kuna wengi ambao wamejipanga vizuri, wamekuwa katika sekta hii kwa muda mrefu na wamejiendeleza. Wameendesha maisha yao vizuri na wametengeneza Sacco yao . Ijapokuwa walianzia kwa kuandikwa kama waendeshaji wa bodaboda, kwa sababu ya uadilifu wao, wameweza kununua bodaboda zao binafsi. Hao ni wale wamejipanga. Lakini kuna wachache wanaoharibu jina la sekta hii kwa kuingiza uhuni na kufanya mambo yasiyostahili. Wahalifu wengi wanaohusika katika uporaji wa mali ya watu na majangili wanaohusika na visa vya mauaji, hutumia bodaboda wakati mwingi kutekeleza uhalifu huo. Wengi wanaofanya kazi ya bodaboda wanafanya kazi nzuri sana na wanastahili kuungwa mkono. Kama nchi, ni muhimu tutunge sheria ambazo waendeshaji wa bodaboda watafuata. Sisi kama watumizi wa barabara, huwa tunawaona waendeshaji wa bodaboda wakivunja sheria za barabara. Unajipata unaendesha gari lako katika ule mkono wako wa kulia wa barabara lakini mtu wa bodaboda anaupitia mkono huo huo bila kujali kuwa anaweza kusababisha ajali. Tumeona mara nyingi sana katika barabara zetu ajali nyingi zilizosababishwa na watu wa bodaboda. Watu wasiostahili kupoteza maisha yao wameyapoteza kwa sababu ya waendeshaji wa bodaboda kutokuwa na umakini. Hili ni jambo sugu katika nchi yetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
        },
        {
            "id": 1561789,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561789/?format=api",
            "text_counter": 577,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Ganze, PAA",
            "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
            "speaker": null,
            "content": "Katika mahospitali ya Kaunti za Kilifi na Malindi, kuna wadi zinazoitwa Bajaj Wards. Watu wanaopatikana katika wadi hizo ni wale waliopata ajali kupitia bodaboda. Kwa hivyo, bali na kuwa wamefanya kazi nzuri, wachache wasio na umakini wamesababisha hasara kubwa sana. Itabidi watu hospitalini wafanyiwe operesheni na kuwekewa vyuma. Wakati mwingi utapata hawana pesa za matibabu na inatubidi sisi kama wanasiasa tufanye michango ili wasaidike."
        },
        {
            "id": 1561790,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561790/?format=api",
            "text_counter": 578,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Ganze, PAA",
            "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
            "speaker": null,
            "content": "Naunga mkono. Hata kama umeondolewa katika Bunge hili, nasisitiza kuwa ikiwezekana, Kamati husika iregeshe Mswada huu ili tuwe na sheria ambazo zitazingatiwa ili tuhakikishe kuwa manufaa ya sekta ya bodaboda yanasikika katika kila kona ya nchi hii. Impact ya sekta hii inaonekana kwa sababu wamerahisisha sana usafiri nchini mwetu. Lakini kwa sababu ya wale wachache ambao hawazingatii sheria, jina la watu wa bodaboda limeharibiwa sana. Kitendo cha uhalifu kikifanyika kule mashinani, mshukiwa wa kwanza huwa ni mtu wa bodaboda. Kwa hivyo, ni wakati mwafaka kwa zile asasi za Serikali zinazohusika kama vile"
        },
        {
            "id": 1561791,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1561791/?format=api",
            "text_counter": 579,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "National Transport and Safety Authority (NTSA)"
        }
    ]
}