GET /api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=155180
HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "count": 1608389,
    "next": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=155181",
    "previous": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=155179",
    "results": [
        {
            "id": 1569992,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569992/?format=api",
            "text_counter": 204,
            "type": "other",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": ". Cha muhimu ni kwamba we are whitelisted by IMO. So, we arein a positive space. I submit"
        },
        {
            "id": 1569993,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569993/?format=api",
            "text_counter": 205,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Kingi",
            "speaker_title": "The Speaker",
            "speaker": null,
            "content": " Sen. Miraj, please, proceed."
        },
        {
            "id": 1569994,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569994/?format=api",
            "text_counter": 206,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Miraj",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Bw. Spika, kwanza niruhusu nimpongeze Waziri wetu kwa kuona kwamba vyeti vyetu sasa vinatambulika na mataifa manne ikiwemo Korea. Juzi, tumeona katika Facebook page yao kwamba wameweza kusign pamoja na Italy. Lakini, swali hili nimeuliza kwa mara ya pili. Niliuliza awamu ya Mvurya aliyekuwa Waziri katika Wizara hii hii na nimeliuliza tena. Sababu ya kuuliza swali hii tena ni kwamba jamii zetu za pwani hazitononoki jumla ya kuwa tunaona kwamba---"
        },
        {
            "id": 1569995,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569995/?format=api",
            "text_counter": 207,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Kingi",
            "speaker_title": "The Speaker",
            "speaker": null,
            "content": " Sen. Miraj, what is your question?"
        },
        {
            "id": 1569996,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569996/?format=api",
            "text_counter": 208,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Sen. Miraj",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Swali langu ni, jamii za Pwani ambazo zinategemea uchumi samawati ikiwemo uvuvi na fedha ambazo zinashirikiana na bahari, tunaona kwamba hundi zinapeanwa mara nyingi na hata Rais anapokuja Pwani, tunaona miradi nyingi anazosimamia ni miradi ya uchumi samawati. Lakini kila wakati tunapouliza fedha zile zinawafikia kina nani, hatupati majibu. Leo, Waziri amesema wazi ya kwamba hawana ufahamu ni akina nani wamekuwa wakipokea pesa hizi. Je, tutawaambia nini Wapwani kuhusiana na zile hundi za fedha ambazo tunaona zinaendelea kupeanwa na hatujui wanaozipokea ni akina nani? Pili, kwenye upande wa uvuvi, ningependa kumwuliza Waziri, ndugu zetu wanapopata ajali katika maji, wanapozama wakiwa kazini wanavua, kuna mikakati gani kuona kwamba wanapata chombo kama helicopter, ili wakati ajali zile zinatokea, wanaweza kukimbia na kuwapa huduma ya kwanza haraka? Asante, Bw. Spika."
        },
        {
            "id": 1569997,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569997/?format=api",
            "text_counter": 209,
            "type": "speech",
            "speaker_name": "Hon. Kingi",
            "speaker_title": "The Speaker",
            "speaker": null,
            "content": " Waziri unaweza kujibu. Ningependa kukujulisha kwamba ukiamua kujibu swali kwa kimombo, lazima uendelee kwa kimombo, ukiamua kujibu swali kwa Kiswahili, utaendelea na Kiswahili. Usichanganye lugha hizo mbili wakati unajibu. Endelea Waziri."
        },
        {
            "id": 1569998,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569998/?format=api",
            "text_counter": 210,
            "type": "other",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "The Cabinet Secretary for Mining, Blue Economy and Maritime Affairs"
        },
        {
            "id": 1569999,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1569999/?format=api",
            "text_counter": 211,
            "type": "other",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "(Hon. Hassan Ali Joho): Asante kwa ujuzi. Nilikuwa najua ni vile maneno mengine yako na changamoto. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
        },
        {
            "id": 1570000,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570000/?format=api",
            "text_counter": 212,
            "type": "other",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "Miradi iko tofauti ya uwazi wa Serikali na vyombo visivyokuwa vya Serikali. Hii Shilingi 1 billioni ambayo umesema ni pesa ambayo imepitia NGO, wamepata rasilmali kupitia Serikali na ufadhili wa Canada. Imekuwa changamoto kwetu kuwauliza hii NGO itupatie hesabu na uwazi kwa sababu wako na tabia na mienendo zao. Lakini zile za Serikali, niko tayari kueleza kinaga ubaga kwamba tumepeana takriban Shilingi 3.2 billioni kwa vikundi tofauti vya akina mama na vijana, kunua maboti. Tumenunua maboti takriban 129, tumejenga bahari za uvuvi chache, tisa hivi. Wakati huu tunajenga katika Lake Victoria, tumejenga zingine tano katika jimbo la Pwani, zingine bado zinaendelea, zingine tumeadvertise juzi na kadhalika. Kuhusu jambo la ajali, ningependa kusema kwamba wale watu ambao unawaita watu wako ni watu wetu sisi wote. Kwa sasa hivi, ukienda Lamu, Mombasa, Kilifi na Kwale, utakuta tumewapatia boti la kuokoa watu la uwepesi, lenye mwendo wa kasi, la kisasa. Lakini, ninakubaliana na wewe kwamba katika mipango za siku za usoni, tunataka kuekeza katika teknolojia mpya ya kutumia drones na helicopter. Hiyo iko katika mipango kabambe ambayo tumeweka. Tukitathmini kwa kina, utakuta kwamba hiyo ndiyo njia mwafaka ya kufuata."
        },
        {
            "id": 1570001,
            "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570001/?format=api",
            "text_counter": 213,
            "type": "scene",
            "speaker_name": "",
            "speaker_title": "",
            "speaker": null,
            "content": "I submit."
        }
    ]
}