HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=157019",
"previous": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=157017",
"results": [
{
"id": 1588372,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588372/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "scene",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Loud consultations)"
},
{
"id": 1588373,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588373/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi North, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi kuunga hoja ya makubaliano ya Bunge kuhusu Mswada huu. Niseme kwamba huu ni Mswada muhimu sana. Ninampongeza Mhe. Ruweida Mohamed kwa kujali watu wake wa Lamu na Pwani. Hawa wanyama tunaowaweka katika ratiba ya wale ambao wakiumiza watu watalipwa fidia ni viumbe walioko baharini. Viumbe hawa wamekuwa wakiwadhuru sana watu wa Lamu, kwani wengi wao hupata chakula chao cha kila siku kupitia Bahari ya Hindi."
},
{
"id": 1588374,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588374/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi North, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Ruweida Mohamed, ningependa kusema kwamba umefanya kazi nzuri sana. Watu wa Pwani na Lamu watakukumbuka maisha yao yote kwa kazi hii nzuri uliowafanyia kupata fidia wanapopata hasara ndani ya bahari."
},
{
"id": 1588375,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588375/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi North, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "Naunga mkono makubaliano na hoja hii ambayo Mhe. Ruweida Mohamed amewasilisha."
},
{
"id": 1588376,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588376/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi North, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
},
{
"id": 1588377,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588377/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Peter Kaluma",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": " Hon. Rachael Nyamai, in terms of procedure, the Question has to first be put."
},
{
"id": 1588378,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588378/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "scene",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Question proposed)"
},
{
"id": 1588379,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588379/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Peter Kaluma",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai."
},
{
"id": 1588380,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588380/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui South, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika wa Muda, ningependa kuchukua fursa hii kumpa kongole Mheshimiwa wa Lamu Mashariki, Mhe. Ruweida Mohamed. Amefanya kazi nyingi sana. Kwa kawaida, Mhe. Ruweida Mohamed anajali watu wake wa Lamu, hususan kuhusu mambo yanayohusu bahari na umbali kutoka Nairobi. Tumemsikia akiwa Bungeni akisisitiza jinsi anavyopenda kuhakikisha kuwa watu wake wanapewa fidia, hasa kwa mambo yanayohusu bahari."
},
{
"id": 1588381,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588381/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui South, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
"speaker": null,
"content": "Ningependa pia kumpongeza Mhe. Owen Baya, na nimwambie kuwa nimeona Kiswahili kimeanza kumshinda. Sijui ni kwa sababu gani, au labda kutokana na kukaa sana na Mhe. Kimani Ichung’wah, Mhe. Silvanus Osoro na Mhe. Naomi Waqo. Huwa wanamwongelesha Kiingereza mingi hadi siku hizi ameanza kusahau Kiswahili."
}
]
}