{"id":1014963,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1014963/?format=json","text_counter":481,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Mradi wa MES ulikuwa na lengo nzuri sana. Tulipoenda Tana River, tuliona kuwa vifaa vingine vilikuwa pale kama vile Computerized Tornography (CT) scan na X-Ray. Vifaa vinatumika ingawa kuna uhaba wa wataalamu. Kwa mfano, X-Ray na CT scan zao zilikuwa ni lazima kupelekwa Mombasa kusomwa na kurejeshwa Tana River ili watu waweze kuhudumiwa."}