{"id":1019046,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1019046/?format=json","text_counter":116,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"na Kamati ya Justice, Legal Affairs and HumanRights kuhusu mambo ya mipaka kule Taita-Taveta. Mpaka sasa sijapata majibu. Taarifa hiyo ilikua inauliza kuhusu mpaka wa Taita-Taveta na Makueni kwa sababu ya ule mtafaruku ulioanza kati ya Serikali ya Kaunti ya Makueni na Taita-Taveta. Nilisema kuwa katika District and Boundaries Act ya 1992, wakati wa kuelezea mipaka ya Wilaya ya Makueni ilisema kwamba Mtito Andei iko Makueni na ikasema tena kuwa iko Taita-Taveta."}