{"id":1037247,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037247/?format=json","text_counter":615,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Waheshimiwa Maseneta, tunajua kwamba kutokana na janga kuu la COVID-19 katika Mwezi huo tu wa Machi, shughuli zetu zilikuwa haziwezi kuendeshwa vizuri kwa sababu mabunge yote ulimwenguni yalianza mikakati ya kuhakikisha kwamba yanachunga kuenezwa kwa ugonjwa wa COVID-19 kati ya Wabunge wenyewe na wafanyikazi wa Mabunge hayo."}