{"id":1037885,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037885/?format=json","text_counter":287,"type":"speech","speaker_name":"Kisumu West, FORD-K","speaker_title":"Hon. Olago Aluoch","speaker":{"id":5,"legal_name":"John Olago Aluoch","slug":"john-aluoch"},"content":" Bw. Spika, Alhamisi wiki jana, niliamua kuonyesha uzoefu wangu wa lugha yetu ya taifa; Kiswahili. Lakini kuna Wabunge kama Mhe. Millie Odhiambo waliolalamika kuwa nilikuwa ninawatesa kwa kuongea kwa lugha ya Kiswahili. Kwa sababu hiyo, nimeamua kuwa leo nitaonyesha uzoefu wangu kwa lugha ya Kiingereza."}