{"id":1043199,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1043199/?format=json","text_counter":171,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Vilevile katika Kifungu cha tisa, World Anti-Doping Agency (WADA) itakuwa taasisi huru katika nchi ambayo haitaegemea upande wowote kwa Serikali ama kwa shirika lolote la michezo katika kutekeleza jukumu lake. Hii ni muhimu kwa sababu bara nyingine itakuwa inalemea upande mmoja na federation fulani. Ina maana kwamba hawataweza kutoa uamuzi huru katika masuala muhimu kama haya."}