{"id":1053939,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1053939/?format=json","text_counter":145,"type":"speech","speaker_name":"Mvita, ODM","speaker_title":"Hon. Abdullswamad Nassir","speaker":{"id":2433,"legal_name":"Abdulswamad Sheriff Nassir","slug":"abdulswamad-sheriff-nassir"},"content":"Mwishowe nikimalizia, kuna huu mwenendo wa Katiba 2010 ambao Waziri anaandika ripoti, kisha anampelekea Mjumbe kuisoma. Nasikitika itabidi waregeshe tena suala hili ili wajue ukweli. Mwisho, wamesema post-mortem ilifanywa. Hakuna post-mortem yeyote ilifanywa kwa marehemu. Kwa hivyo, nasikitika kwa sababu itabidi dadangu ambaye yuko katika Kamati ambayo inahusika arejee tena kuambia Serikali kuwa kuna kiwango ambacho watu wanaweza kuhadaiwa."}