{"id":1059628,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1059628/?format=json","text_counter":74,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":"Tumeona ya kwamba tumepoteza madaktari wa ngazi za juu kwa ugonjwa huu wa COVID-19 ambao bado tunawahijati katika nchi hii. Ukiangalia idadi ya wale waliofariki katika ulimwengu ni madaktari, wauguzi, na wanafanya kazi hospitalini. Hao ndio walioathirika sana na ugonjwa wa COVID-19."}