{"id":1066861,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066861/?format=json","text_counter":74,"type":"speech","speaker_name":"Mhe. Samia Suluhu Hassan","speaker_title":"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania","speaker":null,"content":"Tunatambua kwamba kila nchi - ikiwemo Tanzania - imejiwekea utaratibu wa kupambana na janga hili kulingana na mazingira yake mahsusi na hali ya kusambaa kwa ugonjwa huo katika nchi hizo."}