{"id":1066966,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066966/?format=json","text_counter":62,"type":"speech","speaker_name":"Mhe. Samia Suluhu Hassan","speaker_title":"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania","speaker":null,"content":"Hivi ndivyo majirani na ndugu walioshibana wanavyoishi. Yeyote anayefikiria ama kudhamiria kuleta uhasama baina yetu, ujumbe kwao ni kuwa, Tanzania na Kenya tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo. Iwe kiangazi; iwe masika, Tanzania na Kenya tupo."}