{"id":1068904,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068904/?format=json","text_counter":122,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Asante Bw. Spika kwa fursa hii ya kuchangia Mswada wa Marekebisho ya Katiba ulioletwa katika Seneti. Kwanza, ningependa kuwapongeza waasisi wa Mswada huu kwa kutupa fursa ya kurekebisha Katiba yetu wakati tuna amani na hakuna msukosuko wowote katika Jamhuri ya Kenya."}