{"id":107253,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/107253/?format=json","text_counter":249,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Mwadeghu","speaker_title":"","speaker":{"id":98,"legal_name":"Thomas Ludindi Mwadeghu","slug":"thomas-mwadeghu"},"content":"Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika. Sioni kuwa Waziri Msaidizi anachukulia hili jambo vile linavyohitajika kuchukuliwa. Kama alienda Malindi na akaona ile hali ya taharuki iliyokuweko; watu wanataka kuuana, na huku anasema hamna lolote la taharuki. Waziri Msaidizi anafanya fedheha kwa watu wa Mkoa wa Pwani na naomba ikome!"}