{"id":1083999,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1083999/?format=json","text_counter":156,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wario","speaker_title":"","speaker":{"id":13224,"legal_name":"Golich Juma Wario","slug":"golich-juma-wario"},"content":"Ingekua vyema kama Serikali ingetenga pesa za kutosha ili wananchi wetu wapate chanjo. Hii ni kwa sababu kama wananchi hawatapata chanjo na hakuna tiba ya COVID-19, basi hofu tuliyonayo wakati huu itaendelea kutandaa na itafanya uchaguzi usiwe wa maana kwetu."}