{"id":1089855,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1089855/?format=json","text_counter":68,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Bi. Naibu Spika, sikutaka kuongea kuhusu hili jambo. Lakini, ninajua kwa nini amekosea. Nimekuwa nikimfuatilia kwa mambo ya mgongo wa chupa. Amefanya makosa kwa sababu, wakati sisi tunasema mambo kwa kingereza ‘ bottom up’, nimekuwa nikimskia akisema. Ndio maana amefanya makosa hayo na ninamuelewa."}