{"id":112249,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/112249/?format=json","text_counter":306,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Sisi tumekuwa katika hoja kama hii wakati ule wa mwisho wa kutafuta Katiba. Tulikaa hapa mpaka usiku wa manane, lakini tulikuwa tunapigana; tulikuwa hatufanyi maridhiano. Kwa wakati huu, Wakenya wameamua ya kwamba lazima tupate Katiba. Na sisi Wabunge tumeamua kwamba, hata watuambie nini huko nje; watuseme, watuandike, watufanyeje, watutukane--- Wengine wanasema--- Eti leo katika gazeti moja ambalo Mbunge amezungumzia hapa---Gazeti limesema tunakataa kupitisha Katiba kwa sababu tunangoja ridhaa. Ni haki gani kuzungumza mambo kama hayo; kuleta madharau kwa Bunge letu? Wakati unaandika mambo hayo, ndio gazeti lako litanunuliwa na tutakupigia makofi lakini, kumbuka ukivunja hadhi na heshima ya Bunge, unajiumiza wewe kama Mkenya wa kawaida."}