{"id":1137507,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1137507/?format=json","text_counter":438,"type":"speech","speaker_name":"Elgeyo/Marakwet CWR, JP","speaker_title":"Hon. (Ms.) Jane Chebaibai","speaker":null,"content":" Watu wameuawa na wenzao, lakini hakuna mtu amechukua maanani kabisa. Leo tumekuja kuketi hapa ili watu watutukane. Tumekuja kuketi hapa tuzungumzie mambo ambayo yanadhulumu taifa la hustlers . Tumenyanyaswa kwa muda mrefu katika taifa la Kenya. Watu wa Elgeyo/Marakwet na Kerio Valley wamekufa. Tumezungumzia jambo hilo hapa, lakini hakuna mtu anatia maanani. Naona tunapoteza wakati leo."}