{"id":1159409,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1159409/?format=json","text_counter":96,"type":"speech","speaker_name":"Lamu CWR, JP","speaker_title":"Hon. (Ms.) Ruweida Obo","speaker":{"id":786,"legal_name":"Ruweida Mohamed Obo","slug":"ruweida-mohamed-obo"},"content":"Tukiunda hizi sheria, tufikirie kuna sehemu zingine hapa Kenya ambazo mpaka sasa hazina hata Wi-Fi . Tukizungumzia kuhusu kufungua Kenya kwa dunia nzima, tufikirie zile shule ambazo bado zinatumia tarakilishi, lakini hazina network ama hata Wi-fi . Nyinyi wataalamu katika sekta ya ICT na Kamati wachukue nafasi kuzingatia hayo. Wengine wamepelekwa mbele zaidi na pengo litakuwa kubwa sana. Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."}