{"id":1163537,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1163537/?format=json","text_counter":50,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":"Bi. Naibu Spika, ijapokuwa hawa ni watu wa chama, kuzingatia harakati zao ni kwamba waliweza kuachishwa kazi. Hili ni jambo la kusikitisha sana; kuleta hali ya uchumi mbaya kwenye nyumba za walimu. Walimu hawa wana taaluma ambayo walimu wengine hawana. Wanaanza kufudisha watoto wakiwa bado ni wachanga sana wakati hawajua chochote ikiwemo kusoma."}