{"id":1192130,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192130/?format=json","text_counter":147,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Sifuna","speaker_title":"","speaker":{"id":13599,"legal_name":"Sifuna Edwin Watenya","slug":"sifuna-edwin-watenya"},"content":"Bw. Spika, naamini ya kwamba Seneta anaposimama kuzungumza hapa, lazima aweze kuzungumza maswala ambayo anaweza kudhibitisha. Sidhani ya kwamba Seneta wa Kaunti ya Mombasa - ambaye namheshimu sana - anaweza kutoa idhibati yoyote kuonyesha kwamba uvutaji wa bhangi unapelekea watu kuruka vichwa. Hiyo ndiyo hoja yangu ya nidhamu."}