{"id":1193555,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193555/?format=json","text_counter":280,"type":"speech","speaker_name":"Kisauni, ODM","speaker_title":"Hon. Rashid Bedzimba","speaker":{"id":13383,"legal_name":"Ali Menza Mbogo","slug":"ali-menza-mbogo"},"content":". Ni yeye mwenyewe ataenda kwa wananchi na kuwauliza wanataka awafanyie nini na pesa zao. Hana sababu ya kwenda kuombaomba. Tupewe uwezo wa kutumia hii NG-CDF kuwalipa hata wale wazee wa mtaa ambao hawalipwi chochote. Tuweze kuwalipa hata kama ni kitu kidogo kupitia hazina hii ya NG-CDF. Imewasaidia walala hoi. Wazee wa mtaa pia ni miongoni mwa watu wanaotatua kesi nyingi na kusaidia katika masuala ya usalama katika maeneo yetu. Ajabu ni kwamba hakuna kitu wanacholipwa. NG-CDF ni chombo muhimu sana. Hivi sasa, shule za umma zina magari ya kuwazungusha watoto katika ziara za elimu kwa sababu ya NG-CDF. Ingekuwa hakuna NG- The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."}