{"id":1204058,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1204058/?format=json","text_counter":511,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Kwa hivyo, mpaka sasa na kulingana na stakabadhi zilizotolewa ni kwamba chama cha UDM bado kiko katika mrengo wa Azimio-One Kenya. Sheria inawatambua kama wanachama wa mrengo wa Azimio-One Kenya mpaka watakapojitoa katika mrengo huo. Kwa sababu hiyo, mwanachama wa mrengo wetu hawezi kupendekezwa na upande wa pili."}