{"id":1211159,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1211159/?format=json","text_counter":156,"type":"speech","speaker_name":"Migori County, Independent","speaker_title":"Hon. Fatuma Mohammed","speaker":null,"content":" Shukran Mhe. Spika wa Muda. Nimeamka kuitetea NG-CDF na NGAAF. Kama mwakilishi wa kina mama, najua vile pesa tunazopata kupitia NGAAF zinawasaidia walio mashinani. Kusema kweli, watu mashinani wanajua NG-CDF na NGAAF lakini imesemekana haiko kwenye Katiba. Hili ni jambo ambalo wananchi wakilisikia watapata uchungu. Kutokana na mambo mengi ambayo yamezungumzwa, NG-CDF na NGAAF ni kama kanisa; usipoipata hauna maisha. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."}