{"id":1215685,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1215685/?format=json","text_counter":113,"type":"speech","speaker_name":"Matuga, ANC","speaker_title":"Mhe. Kassim Tandaza","speaker":null,"content":" Asante, Mhe. Naibu Spika. Kuna watoto wa shule ambao wanatusikiza tukizungumza Kiswahili. Mhe. Babu Owino alisema kwamba kuna nguo ambayo imekaa kwekwe kwekwe . Hicho si Kiswahili sanifu. Huenda Watoto wetu wakalichukulia kuwa neno hilo litaingia katika Kamusi kwa sababu ni Waheshimiwa wamelitaja. Ningeomba hilo neno litolewe na wanafunzi wajue kwamba hakuna neno kama hilo lililotumiwa na Mhe. Babu Owino. Asante."}