{"id":1219543,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219543/?format=json","text_counter":165,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Bw. Spika, hospitali hii ndio tumaini la wananchi wengi katika eneo zima la Pwani, kwa hivyo, ni muhimu iweze kutoa huduma bora ili kuokoa maisha. Kwa hivyo, ningeomba Taarifa hii iwasilishwe kwa Kamati ya Kudumu ya Afya na walichunguze swala hili kwa undani ili mambo yaliyoshuhudiwa juzi yasirudiwe. Asante, Bw. Spika."}