{"id":1222992,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1222992/?format=json","text_counter":91,"type":"speech","speaker_name":"Nyali, UDA","speaker_title":"Hon. Mohammed Ali","speaker":null,"content":"Kisha angalia vijikike viwili vimesimama kando ya barabara vikifanya vile vile. Siku hizi hawana hata haya; hawana aibu. Wanachapisha vitabu na kuweka picha zao mitandaoni wakisema, “ I am in love”. Lo! I am in love kiatu changu! Hatutakubali tabia hiyo sisi kama Wabunge. Hatutaikubali kama nchi. Hii nchi ina Mungu na ina dini."}