{"id":1223085,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1223085/?format=json","text_counter":184,"type":"speech","speaker_name":"Luanda, DAP-K","speaker_title":"Mhe. Dick Oyugi","speaker":null,"content":"Mhubiri mmoja na mwandishi wa vitabu vingi anayejulikana kama Myles Munroe – ambaye alituacha hivi majuzi – aliandika vitabu vingi sana kuhusu maadili mazuri katika maisha ya mwanadamu. Katika kitabu kimoja, alizungumzia mambo ya ushoga, na akasema kuwa ushoga ni jambo geni; ni jambo la aibu na si nzuri. Ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa nyuma ya pazia, lakini sasa limewekwa wazi. Ushoga haukubaliki na haustahili kukubaliwa katika nchi yetu."}