{"id":1236738,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236738/?format=json","text_counter":407,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"ambayo imekuja sasa hivi na tunataka kupitisha, inaendelea kunyima Kaunti yangu ya Taita-Taveta fedha. Wakati wa mfumo wa kuangalia maeneo ambayo yatafaidika kwa pesa ya kusawazisha magatuzi, Kaunti ya Taita-Taveta ilikuwa inafaidika. Wakati wa kupitisha mfumo wa kugawanya hizi pesa kwa mara pili, yaani second generation, tulipata kwamba Kaunti ya Taita-Taveta imepewa Wadi mbili peke yake. Hizo Wadi mbili ni Kasighau na Chala. Wadi mbili kati ya Wadi 20 za Kaunti ya Taita-Taveta."}