{"id":1236773,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1236773/?format=json","text_counter":442,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Nashukuru sana, Bi. Spika wa Muda. Ninaongea kuhusu uhitaji wa wananchi ama eneo la Taita-Taveta wa hizi pesa za usawazishaji wa magatuzi. Bi. Spika wa Muda, kuna maeneo yalioachwa nyuma kimaendeleo na Taita- Taveta ilikuwa ni kati ya hayo maeneo. Hiyo pesa ilioekewa uwa ama kwa kimombo ilikuwa ring-fenced, ni ya kupeleka madawa hospitali, kupelekea wananchi maji, stima na kujenga barabara. Je, leo hii, wakati wa mfumo wa kugawanya hizi pesa kwa awamu ya pili, kuwacha Taita-Taveta inamaanisha ya kwamba Taita-Taveta imepata barabara?"}