{"id":1266858,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1266858/?format=json","text_counter":51,"type":"speech","speaker_name":"Sen (Dr.) Murango","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Asante, Bw. Spika. Ninachukua fursa hii kuwakaribisha wanafunzi kutoka shule ya Thumaitha. Thumaitha ni mojawapo ya shule ambazo zinajikaza kisabuni katika masomo, wakielewa kwamba masomo tu ndio yanaweza kusawazisha mahuluku-taabu, yaani hustlers, na matajiri na wakae meza moja. Kwa hiyo, ninawapa walimu kongole kwa kuhakikisha kwamba hawa wanafunzi wamefika hapa siku ya leo. Asante."}