{"id":1276264,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1276264/?format=json","text_counter":325,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Kule kwetu, Kaunti ya Taita Taveta, tuna shida ya mipaka kati ya Taita Taveta na Kwale; Taita Taveta na Makueni na Taita Taveta na Kajiado. Nimeleta mara zaidi ya mia katika hili Bunge, swala la kuangazia mipaka kati ya Taita Taveta na kaunti ambazo ni jirani."}