{"id":13223,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/13223/?format=json","text_counter":275,"type":"speech","speaker_name":"Mr. Kutuny","speaker_title":"","speaker":{"id":61,"legal_name":"Joshua Serem Kutuny","slug":"joshua-kutuny"},"content":"Lakini vile vile, ngoja ngoja huumiza matumbo. Ningependa umshurutishe Waziri – na siyo kuomba wakati huu – awasilishe Taarifa hiyo. Mikahawa ilivamia tarehe 23/2/2011. Mkahawa mwingine ulivamiwa tarehe 2/1/2011. Tena, tarehe 10/4/2011 mkahawa mwingine ulivamiwa. Juzi, mkulima maarufu aliuwawa na majambazi. Sasa, tunataka Taarifa hiyo."}