{"id":1342375,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1342375/?format=json","text_counter":274,"type":"speech","speaker_name":"Magarini, ODM","speaker_title":"Hon. Harrison Kombe","speaker":null,"content":"Vile vile, Halmashauri ya Barabara Kuu inafaa kutekeleza mpango wake: barabara kutoka Marikebuni kuingia Ngarashi mpaka Baricho iweze kuinuliwa hadhi yake na kupata lami. Ni mipango ambayo yapo, lakini ikiwezekana, tungeomba fedha zile za mwaka 2023/2024 ziachiliwe mara moja ili kazi hizi ziendelee. Hayo yakifanyika, ninatumai kwamba kila mmoja atafurahia kazi njema inayoendelea."}