{"id":138146,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/138146/?format=json","text_counter":594,"type":"other","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Bi Naibu Spika wa Muda, maswala yote tukiyazungumzia; sio Mau peke yake, bali kila mahali, imefika wakati ambapo Waziri anayehusika na maswala ya mazingira, haswa Waziri Michuki--- Najua kwamba kwa vile yeye ni chapa kazi, ataweza kulitenda jambo hili. Ni muhimu apewe pesa za kutosha ili aweze kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanazidi kuwa mazuri na yaache kuzoroteka."}