{"id":1404480,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1404480/?format=json","text_counter":264,"type":"speech","speaker_name":"Malindi, ODM","speaker_title":"Hon. Amina Mnyazi","speaker":null,"content":"Ardhi nyingi kule Malindi zimezuiliwa na mabwenyenye - watu ambao hatuwatambui na hatujui walipata ardhi Malindi vipi. Mara nyingi, tumeona watu wangu wa Malindi wakivunjiwa manyumba yao na kudhulumiwa kwa njia moja ama nyingine."}