{"id":144264,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144264/?format=json","text_counter":157,"type":"speech","speaker_name":"Bi. Leshomo","speaker_title":"","speaker":{"id":379,"legal_name":"Maison Leshoomo","slug":"maison-leshoomo"},"content":"Bw. Naibu Spika, ningependa kumwomba Waziri Msaidizi asiseme eti ni bomu moja liko huko kwa sababu mabomu mengi yako huko. Nina thibitisho kwamba mabomu yameonekana katika eneo hilo la Nairoborkeu . Je, hii familia iliyoathirika italipwa kwa njia gani? Je, mali iliyoharibika italipwa? Kuna watu wengi ambao wamehama mashamba yao kwa sababu ya mabomu yaliyomo ardhini."}