{"id":1446089,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1446089/?format=json","text_counter":223,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"s. Kamati pia ziliweza kufanya kazi nyingi wakati wa janga la COVID-19 walipokuwa wakifanya mikutano online ili kuhakikisha kwamba kazi ya Bunge inaendelea kufanyika bila shida yoyote. Vile vile, wakati wa COVID-19, tuliweza kufanya mikutano na watu kutoka nchi mbalimbali tukiwa hapa nchini. Hivyo basi, tuliweza kupunguza gharama za usafiri na kufanya mikutano kwa kiasi kikubwa. Maswala ya e-Parliament yatasaidia kupunguza gharama za Bunge itakapoanza kutumika kikamilifu. Bi. Spika wa Muda, kwa hayo mengi, asante kwa kunipa fursa hii ili kuunga mkono ripoti hii."}