{"id":1476051,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476051/?format=json","text_counter":440,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Sheria ya DORA ilipitishwa mapema mwaka huu. Kiwango cha pesa zinazotakikana kwenda kwa kaunti zetu kwa mwaka huu wa 2024/2025 ni shilingi bilioni 400.1. Lakini kutokana na kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa 2024/2025 katika Bunge la Kitaifa, imebidi kufanywe marekebisho ili zile pesa zingekwenda kwa kaunti zetu zipunguzwe kulingana na ukweli kwamba Serikali haitaweza kukusanya pesa kama vile walivyokuwa wanatarajia."}