{"id":1476059,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476059/?format=json","text_counter":448,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Tukiangalie zile sheria ambazo serikali kuu ilipitisha kupitia Bunge hili na Bunge la Kitaifa, utapata kwamba zimeongeza gharama katika kaunti zetu. Kwa mfano; sheria ya afya, Social Health Insurance Fund (SHIF) inaongeza gharama kwa serikali za kaunti kwa sababu mfanyakazi analipiwa na vile vile, pia kaunti inachangia katika pesa zile."}