{"id":1479890,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1479890/?format=json","text_counter":63,"type":"speech","speaker_name":"Kaloleni, ODM","speaker_title":"Hon. Paul Katana","speaker":null,"content":" Mhe. Spika, ndio maana nasema vitengo vya usalama vimelegea. Ni lazima wachunguze kule mihadarati inakotoka kwa sababu hatuna mashamba ya cocaine wala heroin . Wajue ikiwa inakuja kwa njia ya meli ama njia nyingine. Mipaka yetu lazima ilindwe ili tuhakikishe kuwa hakuna mihadarati inayoingia katika taifa letu. Ahsante, Mhe. Spika."}