{"id":1514233,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1514233/?format=json","text_counter":616,"type":"speech","speaker_name":"Wundanyi, WDM","speaker_title":"Hon. Danson Mwashako","speaker":null,"content":"Kungekuwa mfumo kama NG-CDF ungetumika kugawanya pesa ambazo zinachangia mambo ya barabara, maji na pesa ya elimu, basi Kenya yote ingeendelea kwa usawa. Hatungekuwa na maeneo ambayo yamebaki nyuma. Hii hazina ya NG-CDF inatakikana ichungwe si na Wabunge tu, lakini hata Serikali ya Kitaifa inatakikana ijuwe hii ndio hazina pekee ambayo inafikia mwananchi kule mashinani."}