{"id":1514234,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1514234/?format=json","text_counter":617,"type":"speech","speaker_name":"Wundanyi, WDM","speaker_title":"Hon. Danson Mwashako","speaker":null,"content":"Pesa hizo za NG-CDF leo hii zinasomesha watoto ambao hawangeweza kwenda shule. Kwa sababu ya maamuzi yanayofanyika kule mashinani, yanaweza kufikia wale maskini hohe hahe ambao hawangeweza kufanikiwa na ndoto zao za elimu."}