{"id":1545954,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545954/?format=json","text_counter":57,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Kwa hivyo, sisi sote tukubali kwamba ufisadi uko katika gatuzi zetu. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba huu sio ule ugatuzi tuliolilia na kupitisha mwaka wa 2010; wa kupeleka pesa mashinani. Sisi ambao tunatoka katika eneo zilizo na idadi ndogo ya watu hatukuwa tunapata maendeleo kwa sababu tulikuwa tunaulizwa tunaleta kura ngapi katika meza ili watupatie maendeleo."}