{"id":1567672,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1567672/?format=json","text_counter":154,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Hii Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kanda isikomee Kakamega. Ivalie suala hili njuga na kutembelea kaunti zote, ili kubaini miradi iliyokwama ambapo fedha nyingi zimeingizwa wakati hakuna chochote kimepatikana kwa muda wote huu."}