{"id":1570373,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570373/?format=json","text_counter":264,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ninasema hivi kwa sababu Sen. Mungatana alipokuwa akichangia alisema ya kwamba waliokuja nyuma wameleta kuchanganya yaliyokuwa yamezungumziwa hapo asubuhu. La hasha! Si kuchanganya; ni kuleta mwamko mpya, fikira na nguvu mpya. Watu wanapojadiliana, Wazungu husema ni mjinga tu asiyebadilisha mawazo. Wanaoleta mawazo mapya hata wao wanapaswa kusikilizwa."}