{"id":1625485,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625485/?format=json","text_counter":236,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ibara ya 37 ya Katiba ya Kenya inakubali maandamano ya amani. Inavunja moyo sana ukiona watu wanaandamana wengine kwa amani ilhali kuna wahuni. Jambo la kuvunja moyo zaidi ukitembea Nanyuki – kwa sababu kulikuwa na maandamano ya Saba Saba - msichana wa miaka 24 ambaye ni Julia Njoki alishikwa, akapelekwa kortini na kuhukumiwa. Kwa njia isiyojulikana alifia katika seli."}